Kufuatia kutolewa kwa hoja ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), kutaka kuwafungulia mashtaka Wahitimu wa Vyuo Vikuu wanaodaiwa marejesho ya mikopo, Mbunge wa jimbo la Kahama, Jumanne Kishimba amesema jambo hilo linashangaza kwani idadi kubwa ya Wahitimu hawana kazi.

Kishimba amehoji suala hilo Bungeni Jijini Dodoma, wakati akichangia mjadala wa mapendekezo ya mpango wa maendeleo ya Taifa na mapendekezo ya muongozo wa maandalizi ya mpango wa bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2025/26 unaoendelea.

Amesema, “ mimi nipo Kamati ya Elimu, juzi hapabodi ya mikopo walileta hoja kwamba hawapati marejesho kwa watu waliokopa elimu na wanajiandaa kuanzac oparesheni ya kuanza kuwakamata wadaiwa wote hoja yangu ni Bodi ya mikopo alimpa mtu wa chuo hizo pesa mtu wa chuo akampa elimu mwanafunzi elimu ambayo haiajiriki.”

“Sasa anayetakiwa kushtakiwa ni nani ni Mwanafunzi au ni Chuo kwasababu Dunia inabadilika hatuwezi kuendelea na lugha ile ile ya elimu ni ufunguo wa Maisha, sasa hivi Elimu ni bidhaa wameshindwa kuuza kwahiyo mwenye kosa ni bodi ya mikopo,” alifafanua Kishimba,

ZAMECO yalaani usambazwaji wa maudhui yasiyofaa
Elimu ya mpiga kura kutolewa kwa makundi yote - INEC