Swaum Katambo – Katavi.

Wanahabari Mkoani Katavi pamoja na Wadau wa Utamaduni kutoka maeneo mbalimbali wamepatiwa mafunzo ya siku mbili yaliyolenga kuwajengea uwezo kuhusu Uandishi wa Habari za Urithi wa Utamaduni Usioshikika, ili kukuza fursa za kiuchumi kwa Vijana na Wanawake.

Mafunzo hayo ya siku mbili yaliyofanyika mjini Mpanda, yalifunguliwa na Leah Gawaza ambaye alimwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuf na kuwataka kuripoti habari za Urithi wa utamaduni usioshikika uliopo mkoani Katavi, ili kuwavutia wawekezaji kwa lengo la kukuza fursa za kiuchumi kwa wakazi wa mkoa huo.

Alisema anawapongeza waandaaji wa mafunzo hayo TAMCODE kwa kuchagua Mkoa wa Katavi  kufanya warsha hiyo badala ya mikoa mingine, kutokana na jiografia yake ya kuwa pembezoni na kutoa wito kwa taasisi na mashirika mengine kujitokeza mkoani humo.

Naye Ofisa Maendeleo ya Michezo, Utamaduni na Maendeleo ya Vijana Mkoa wa Katavi, Carol Steven alisema mafunzo hayo yamekuja kwa muda muafaka kwa kuwa hivi karibuni wametoka kwenye maadhimisho ya wiki ya Mwanakatavi ambayo ni mahsusi kwa ajili ya kuenzi utamaduni wa mkoa wa Katavi pamoja na fursa zake za kiuchumi.

Alisema, “katika dunia hii leo, miongoni mwa nchi zilizobaki na utamaduni wake mojawapo ni Tanzania, na tusiposhirikiana na wadau wote utamaduni wetu unaenda kupotea, tuwapongeze kwanza kwa kubuni mradi wenu ambao unasema Urithi wa Utamaduni usioshikika, niseme tu ukweli, makabila machache ndiyo yamebaki na utamaduni wao.”

Carol poa alipongeza hatua ya kuwashirikisha wadau wa habari kwa kusema kuwa “kwa dunia ya sasa ili kufanikisha jambo lako na kuwafikia watu wengi zaidi unapaswa kutumia vyombo vya habari, bila wao huwezi kufanikiwa kwa ukubwa”

Mafunzo hayo yalifungwa na Ofisa utamaduni Manispaa ya Mpanda, Bakari Hamza ambaye alimwakilisha mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda na kuwataka wadau wa utamaduni na wanahabari kutobweteka na badala yake kwenda kuyafanyia kazi kwenye jamii.

“Nawashukuru pia wawekezaji kwa sababu wangeweza kwenda kusoti mikoa mingine na kufanya mafunzo haya, lakini wameuchagua mkoa wa katav,hii ni fursa kwetu,” alisema.

Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo wanahabari pamoja na wadau wa utamaduni wameahidi kuyafanyia kazi mafunzo waliyopatiwa ili kuhakikisha jamii hususani wanawake na vijana wanaachana na dhana ya kutegemea ajira Serikalini na kujishughulisha na vitu vyao vya asili kujipatia kipato.

“Kupitia mafunzo haya tumejifunza mambo mengi, tumekwenda ‘field’ tumeona utamaduni usioshikika, tumeona namna gani wakinamama na vijana wameweza kujiajiri kupitia utamaduni usioshikika.”

“Hivyo mafunzo haya yameninufaisha hata mimi nikitoka hapa najua nina kitu cha kufanya, najua utamaduni ni mtaji pia ni biashara na ukitumika vizuri unaweza ukanyanyua kipato cha mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla” alisema Juma Mbonde mdau wa utamaduni.

Kwa upande wake Mwandishi wa Habari wa Radio ya Jamii Mkoani humo, Evath Tumani alisema, “mafunzo haya ni makubwa sana, hatupaswi kuangalia jamii ya upande mmoja,tunatamani kama tulivyonufaika sisi basi tukawanufaishe na wengine kwa sababu tuna tamaduni nyingi ambazo zimepotea kutokana utandawazi, hivyo tutavienzi vitu vyetu vya asili vikiwemo vyakula ili kujenga afya na kutengeneza taifa linalojielewa.”

Warsha hiyo ya siku mbili imeendeshwa na Shirika la Vyombo vya Habari kwa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TAMCODE) kupitia mradi wa UNESCO- Alwaleed Philanthropies.

yanalenga kuwawezesha wanahabari wa redio jamii na mitandao ya kijamii kutumia vyombo vyao kutangaza urithi wa utamaduni usioshikika mkoani Katavi ili kuchagiza fursa za ajira kwa vijana na Wanawake.

Asilimia 99 ya Vijiji vyote nchini vimefikiwa na umeme - Kapinga
Guía Total sobre Casinos bc game en línea