Johansen Buberwa – Kagera.

Ligi ya Samia Cup iliyoanza kutimua vumbi leo Novemba 9, 2024 Mkoani Kagera ambapo timu ya vijana ya soka Manispaa ya Bukoba kuichabanga timu ya vijana soka Muleba goli tano kwa moja katika uwanja wa kaitaba manispaa hiyo.

Mchezo uliochezwa majira ya saa kumi za jioni ndani ya manispaa ya hiyo kweye uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera na mchezo uliochezwa kwa dakika zote 90.

Katika kipindi cha kwanza mchezo ulimalizika kwa timu ya Bukoba ikiongoza goli tatu kwa sifuri na magoli yote kwa upande wa Bukoba goli la kwanza lilifungwa na Renatus Kato dakika ya 28 jezi namba 15 goli la pili Salumu Said
Dakika 33 jezi namba 8 ambaye ni naodha wa timu hiyo.

Goli la tatu Ramadhan Kapilima Dakika ya 43 jezi namba 16 kiungo mshambuliaji la nne Kevin Ishengoma dakika ya 74 jezi namba 7 na aliyepigilia msumali wa mwisho ni Sued Kagutha dakika ya 80 jezi namba 10 kwa upande wa muleba goli moja lilifungwa kipindi cha pili na Franck Femi jezi namba 12 dakika 66.

Awali akizungumza wakati wa ufunguzi wa ligi hiyo mwandaaji Leodiger Kachebinao ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya KPD na ambapo amewaomba vijana wa mkoa huo walioanza kushiri ligi ya Samia Cup wahakikishe wanaonesha vipaji vyao ili waweze kutoka mtaani na kupata furusa ya kwenda kuchezea virabu vikubwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa Kagera Hajjat Fatma Mwassa amewaasa wachezaji kwa kusema mashindano hayo yatakuwa endelevu kwa kuchezwa kila mwaka na kuwata vijana walioshiriki wapambane kuipata zawadi ya mshindi wa kwanza ya milioni kumi pamoja na kuibua vipaji na kuhaidi kuitengeneza timu ya mkoa itakayo tokana na vijana hao.

Ligi hiyo ya Samia Cup itashirikisha timu nane za vijana Mkoani humo yenye lengo la kuhamasisha uchaguzi wa serikali za mitaa novemba 27 mwaka 2024.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Novemba 11, 2024
Kamati yaridhishwa hali ya upatikanaji wa Maji Hanang'