Kamati ya kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI chini ya Mwneyekiti wake, Justin Nyamoga imeelekeza Uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kutekeleza miradi mbalimbali kupitia mapato ya ndani kwani ni miongoni mwa Halmashauri zenye mapato makubwa nchini.
Rai hiyo imetolewa na Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Jafari Wambura Chege kwaniaba ya mwenyekiti wa kamati mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa ghorofa sita wa Hospitali ya Mbagala Rangi Tatu Katika kata ya Mbagala kuu.
Amesema, “kamati inaamini kuwa kupitia mapato ya ndani ya Manispaa ya Temeke mnauwezo wa kukamilisha mradi huu kwa kutumia fedha za ndani na mkawa mfano kwa Halmashauri nyingine zenye mapato makubwa nazo zikaweza kupata somo kupitia Temeke.”
Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa kamati hiyo, Nyamoga hiyo kwa usimamizi mzuri wa miradi mbalimbali ya marndeleo ambayo thamini ya fedha inaonekana katika miradi hiyo.
Kamati hiyo ambayo imefanya ziara yake mkoani Dar es salaam katika Manispaa ya Temeke imetembelea miradi mbalimbali kama vile ujenzi wa shule ya sekondari Magaya, ujenzi wa Bweni na bwalo katika shule ya sekondari Kibasira.
Pia kamati imetembelea na kukagua mradi wa mfereji wa Serengeti na Bwawa la kuhifadhi maji ya mvua kwa Muda na mradi wa ujenzi wa Gorofa sita katika hospitali ya Mbagala rangi Tatu katika kata ya Mbagala kuu.

Kagera: Wanawake TAG wampa Tuzo ya heshima RC Mwasa
LEONBET EDITION yasimamisha jiji kwa burudani ya kibabe