Johansen Buberwa – Kagera.

Umoja wa Wanawake wa Kanisa la Tanzania Assembles Of God (TAG), Kyarunyonga Kata ya Nshambya Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera, wamempatia Mkuu wa Mkoa huo Hajjat Fatma Mwassa tuzo ya heshima na pongezi kwa ajili ya uongozi wake mzuri wa kusimamia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo kuifanikisha Kagera kuwa kinara nchi nzima wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2024.

Mratibu wa Malezi idara ya Wanawake Kanisa la TAG Kata Nshambya Kyarunyonga, Petrida Clavery amesema wanatoa pongezi hizo kutona na utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kimaendeleo ndani ya mkoa huo ikiwemo ujenzi wa miundombinu kupitia sekta ya Maji, Afya, Elimu pamoja kupewa mbolea ya ruzuku.

Amesema kiongozi huyo Mwassa amekuwa mzuri wa kuenzi falsafa za waasisi wa Taifa kupitia mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 mkoa huo umeibuka kidedea kwa kushika nafasi ya kwanza kitaifa kati ya mikoa 31 ambayo ni alama ya Taifa ndani yake inaashiria upendo, Amani,Heshima,matumaini pamoja na kukuza uzalendo kwa hali hiyo anaitenda haki farsafa ya kazi iendelee.

Naye Mkuu wa Mkoa Kagera Hajjat Fatma Mwassa amewashukuru waumini wote wa kanisa la TAG pamoja na Wananchi wote wa kata ya Nshambya kwa kuthamini juhudi na mchango wake kuendeleza mkoa huo maana waumini hao wamejitoa kwa kufunga kwa maombi ndani ya siku saba jambo ambalo sio la kawaida pamoja na kutenga muda wao na kuona umuhimu ya kumtunukia tuzo ya ushidi.

Amesema, “pongezi hizi ziende kwa viongozi wote wakiwemo madiwani na wanachi pamoja na wataalamu wote kwa kushirikiana na kujitokeza kwa wingi maana nyomi ilikuwa ya kutosha kwa ajiri ya kushangilia Mwenge wetu wa uhuru 2024 maana mwaka jana 2023 nilikuta mkoa umeshika nafasi ya 23.

nikawambia wenzagu Mkoa huu mbona mzuri na unafurusa zote sasa tupambane mwaka huu tuitafute nafasi ya tano kitaifa wakati nasema hayo wenzangu wakanishika mkono kwa kunibipu ndo tukasogea mpaka kuishika nfasi ya kwanza.”

Kwa upande Mstahik meya manispaa ya Bukoba Gpyson Godson amesema hii imekuwa historia na rekodi maana tangu mwaka 1961 manispaa hiyo haijawahi kushika nafasi ya tatu kitaifa maana nchi nzima inazohalmashauri 195 bara na visiwani.

Liverpool,Man city ,Arsenal na Chelsea zaingia vitani kuwania EPL
Kamati: Mapato ya ndani yatumike kutekeleza Miradi