Arsenal wako tayari kutumia pauni milioni 83 (euro milioni 100) kumnunua kiungo wa kati wa West Ham Mohammed Kudus huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Ghana mwenye umri wa miaka 24 akitaka kujiunga na The Gunners kucheza soka la Ulaya. (Fichajes – In Spanish}

Tottenham wako tayari kukataa nia mpya ya Real Madrid ya kumnunua beki wa Argentina, Cristian Romero, 26. (Football Insider)

Manchester United wanafikiria kumtoa mshambuliaji wa Uholanzi Joshua Zirkzee mwenye umri wa miaka 23 mwezi Januari huku klabu za Serie A zikimfuatilia. (Calciomercato – In Italy)

Juventus wako mstari wa mbele katika vita vya kumsajili mshambuliaji wa Canada Jonathan David, 24, kutoka Lille huku Manchester United, Liverpool na Inter Milan pia zikimuwania. (Footmercato – In french)

.

Chanzo cha picha,Getty Images

Maelezo ya picha,Jonathan David

Manchester City wameelekeza macho yao kwa mlinda lango wa AC Milan na Ufaransa Mike Maignan, 29.

Borussia Dortmund wanafikiria kumnunua kiungo wa kati wa Sunderland mwenye umri wa miaka 19 Jobe Bellingham Januari. (Alan Nixon via Newcastle Chronicle).

Beki wa Bayern Munich Alphonso Davies yuko tayari kuungana tena na mkufunzi wa zamani Hansi Flick katika klabu ya Barcelona licha ya kutaka kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Canada mwenye umri wa miaka 24 kutoka Real Madrid na Manchester United. (Team Talks)

Kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 31, anakaribia kufikia makubaliano ya kusitisha mkataba wake na Juventus na kusaini klabu nyingine kama mchezaji huru pindi marufuku yake itakapokamilika. (Sky Sports)

.

Chanzo cha picha,Getty Images

Maelezo ya picha,Paul Pogba

Winga wa Ujerumani Leroy Sane ana nia ya kusaini kandarasi mpya katika klabu ya Bayern Munich lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 bado yuko njia mojawapo ya kufikia makubaliano kuhusu mkataba. (Florian Plettenberg),

Beki wa zamani wa Uhispania Sergio Ramos, 38, hatarejea Real Madrid lakini watasajili beki wa kati mwezi Januari, huku beki wa Bayer Leverkusen ya Ujerumani Jonathan Tah, 28, akiibuka kama mgombea mpya. (Diario AS – In Spanish)

Skauti kutoka ndani na nje ya nchi wanafuatilia maendeleo ya Kiano Dyer katika klabu ya Chelsea huku kiungo huyo wa kati wa Muingereza, 17, akikaribia mwaka wa mwisho wa kandarasi yake ya sasa. (Mail)

.

Chanzo cha picha,Chelsea

Maelezo ya picha,Kiano Dyer

Uingereza iko tayari kufanya mazungumzo zaidi wakati wa mapumziko ya kimataifa juu ya kujaribu kuongeza kocha wa makipa wa Chelsea Henrique Hilario kwenye ofisi ya mkufunzi mkuu anayekuja Thomas Tuchel. (Telegraph – Subscription required), nje

David Moyes anatazamia kurejea katika usimamizi wa ligi ya Premier huku Crystal Palace, Wolves, Southampton na Leicester zikimtaka. (Sportsport), nje

Frank Lampard ni mgombea wa nafasi ya meneja iliyoachwa wazi katika klabu ya Championship Coventry City. (Sky Sports)

Polisi: Vijiwe vitumike kupeana maarifa kimaisha si uhalifu
Maisha: Aliyekimbia Mimba yamemkuta makubwa