Vijana wa Kata ya Mtimbira Wilaya ya Malinyi Mkoani Morogoro wametakiwa kupeana mbinu na maarifa yatakayofanya wapate kazi ama shughuli yoyote itakayowaingizia kipato halali na sio kufanya uhalifu, ili kupata pesa.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kituo cha Polisi Mtimbira, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Kajualwake alipokuwa akiongea na vijana waliokusanyika kijiweni wakati wa jioni kwaajili ya kubadilishana mawazo.
Amesema, “vijiwe hivi ni rahisi kuibadilisha fikra ya mtu kutokana na hali tofauti za maisha ya vijana wanaokutana, wapo walioinuka kiuchumi na wale wanaojitafuta ambao ni rahisi kwao kufuata mkumbo, ili mfanikiwe kama wenzenu.”
Kwa upande Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Henry Mwangake, anayefanya kazi katika Kata hiyo amewataka waendelee kumpa ushirikiano kwa kutoa taarifa za uhalifu ili Kijiji chao kiwe salaama.

Tanga: Aliyeibiwa Mil. 10 na mkewe aiangukia Serikali, CCM
Tetesi za usajili Duniani Novemba 12