Swaum Katambo – Katavi.

Serikali imetoa kiasi cha Shilingi Bilion 2.9 kwa ajili ya fidia kwa Wananchi wanaopisha mradi wa Maji kwa Miji 28 katika Bwawa la Milala, ambalo linatekelezwa katika Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko amewashauri Wananchi pindi wapatapo fedha hizo wazitumie kununua ardhi maeneo mengine, ikiwa ni pamoja na kuanzisha makazi mapya huku akisema fedha hizo zisiwe chanzo cha kuleta mitafaruku ndani ya familia.

Amesema, mgao wa fedha hizo utasimamiwa na Wataalamu kutoka Wizara ya Maji, ambao pia watashirikiana na idara ya Ardhi kwa kufuata tathimini iliyofanywa awali, pamoja na wananchi.

Aidha, RC Mrindoko amewaomba Wananchi hao pindi watakapoingiziwa fedha za fidia, kuhama ndani ya siku 90, ili kuruhusu mradi kuendelea.

Madiwani Tanganyika wafanya utambuzi wa maeneo, Majengo
7 Companies Owned by Google Alphabet