Swaum Katambo, Tanganyika – Katavi.
Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Tanganyika Mkoani Katavi limetembelea viwanja na majengo yaliyopo katika Manispaa ya Mpanda yanayomilikiwa na halmashauri hiyo likilenga kuyatambua maeneo hayo.
Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Hamad Mapengo amesema wamefanya ziara hiyo kwa kuwa wengi wao awali hawakuyatambua maeneo hayo na endapo watakwenda kwenye mijadala wapate ufahamu juu ya miradi inayojadiliwa.
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Onesmo Buswelu ameagiza Taasisi na Watendaji wote wanaosimamia miradi ya Serikali kuwa ifikapo Desemba 31, 2024 wawe wamekamilisha miradi yote ambayo ilipaswa kuwa imekamilika.