Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema anatuhumiwa na baadhi ya wanachama wa Chama hicho Mkoani Arusha kwa kuongoza kwa ubabe na kupandikiza watu anaowataka kwenye Nafasi mbalimbali zinazowaniwa katika Uchaguzi wa kuchagua Viongozi mbalimbali wa Chama hicho Kanda ya Kaskazini.

Lema, inadaiwa kuwa amekuwa akiwaweka wagombea hao anaowataka kwa nguvu akijaribu kupanga safu yake kuelekea uchaguzi Mkuu wa 2025, huku akitumia Vijana wa hamasa kuwapiga wanaompinga kwenye teuzi hizo za ndani za CHADEMA, pamoja na kuwasimamisha Viongozi wanaopishana naye kimawazo.

Aidha, Wanachama hao pia wameonesha kusikitishwa na maandalizi ya CHADEMA kuelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024 pamoja na Uchaguzi Mkuu wa 2025, wakishangazwa na namna ambavyo Chama chao kimeshindwa kusimamisha wagombea kwenye maeneo mengi katika uchaguzi wa serikali za Mitaa.

Fill out an ailment facing bc game an internet Casino inside the Canada End Scams
Madiwani Tanganyika wafanya utambuzi wa maeneo, Majengo