Johansen Buberwa – Kagera.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mkoa wa Kagera imeshinda mashauri 17 kati ya 24 kwa kipindi cha miezi mitatu kwa mwaka 2024, huku mashauri 15 yakiwa ni mapya.

Kauli hiyo imetolewa kwa Vyombo vya Habari Mkoani humo hii leo Novemba 14, 2024 na Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa Ezekia Sinkala kwa niaba ya Mkuu wa Taasisi hiyo Mkoa, Vangsada Mkalimoto.

Amesema, kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba 2024, tasisi hiyo imeendelea kutekeleza majukumu yake ambapo uchunguzi wa mashitaka kwa kipindi cha miezi hiyo wamepokea jumla ya Malalamiko 115 na kati ya hayo 50 hayahusu rushwa, hivyo walalamikaji wameelimishwa na kupewa ushauri.

Sinkala ameendelea kusema kuwa, malalamiko 65 yalihusu rushwa na kufunguliwa majalada ya uchunguzi na jarada 17 uchunguzi wake umekamilika na hatua mbalimbali za kisheria zinatarajiwa kuchukuliwa dhidi ya watuhumiwa pamoja na Majalada 48 uchunguzi wake bado unaendelea.

Idadi ya mashitaka hayo 65 N yalihusu Afya, Ushirika, siasa, Fedha, Ujenzi, Aridhi, NHIF, Elimu, Uchukuzi, Uvuvi, Biashara, Viwanda pamoja na Binafsi.

CHADEMA wazichapa hadharani, Lema adaiwa kujimilikisha Chama