Johansen Buberwa – Kagera.

Baadhi ya Madiwani wa Halmashari ya Bukoba Mkoani Kagera, wameiomba Serikali iwalipe Wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii madai yao, ambao walihudumia jamii kipindi cha mripuko wa ugonjwa wa Marburg wa mwaka 2023.

Hoja hiyo imetolewa na Madiwani hao kupitia hoja ya nyongeza wakati wa kuwasilisha taarifa ya kamati ya Elimu, Afya na Maji kwenye kikao cha pili cha baraza la Madiwani kilichofanyika kwenye ukumbi wa Halmashari katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2024/2025.

Diwani wa kata ya Kaibanja, Jasson Rwankomezi na Amatus Makumbo wa Kata ya Kashuaru, wamesema  Wahudumu hao walifanya kazi yao kwa moyo safi na muda wa kulipwa fedha zao umepita na hawaelewi ni lini watapata stahiki zao.

“Wanaodai Marburg pamoja na mhe Diwani kuzumgumzia wanaodai sisi kama Halmashari tungependa kujua idadi ya waliolipwa kwa majina na idadi ya waliobaki kwa majina ili tuwena mwendelezo wa kujua katika halmashauri yetu juu ya swala la marburg,” alisema diwani Makubo.

 

Akitolea ufafanuzi jambo hilo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashari hiyo, Fatna Laay Mganga Mkuu wa Halmashari ya Bukoba Vijijini, Dkt, Bandioti Gavyole amesema wahudumu hao bado wanaendelea kufanya kazi ya kuihudumia jamii na kulitokea matatizo ya akaunti zao za benki ikiwemo baadhi kuisha muda na wengine kukosea namba.

Amesema, “na fedha zikawa zimechukuliwa mwaka huu fedha zikarudishwa na malipo yameanza kufanyika na jambo hilo limeonekana kuzua taharuki lakini kwa wale ambao hawajalipwa watawalipa maana zoezi hilo linaratibiwa na uongozi wa Mkoa.”

Akitoa salamu za Serikali, Mkuu wa Wilaya Bukoba, Erasto Sima amemuagiza Mkurugenzi na Mganga Mkuu wa Halmashari hiyo kuendelea kufuatilia malipo ya wahudumu wa ngazi ya jamii ambao awali idadi yao ilikuwa 1,127.

Watkins afanya kweli Uingereza ikilipa kisasi kwa wagiriki
Uvivu, Uzembe: 56 wapandishwa Kizimbani Mwanza