Ripoti ya Shirika ka Afya Duniani – WHO, inaonesha kuwa kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa surua kiliongezeka duniani kwa asilimia 20 kati ya mwaka 2022 na 2023.

WHO ambayo ilishirikiana na CDC katika ripoti hiyo, imesema takribani watu 110,000 walikufa, wengi wao wakiwa ni watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.

“Milipuko mikubwa zaidi ilitokea katika nchi ambazo watoto walikuwa na lishe bora na wangeweza kustahimili ugonjwa huo na ambako kulikuwa na huduma bora za afya,” ilieleza sehemu ya ripoti hiyo.

Aidha, ripoti hiyo pia imesema surua, moja ya magonjwa ya kuambukiza duniani unaweza kuzuilika kupitia dozi mbili za chanjo kwani asilimia 83 ya watoto hupatiwa chanzo ya kwanza lakini ni asilimia 74 wanaopokea chanjo ya pili ulimwenguni.

Tetesi za usajili Duniani Novemba 15
TANZIA: Pumzika kwa amani King Kikii wa Kitambaa cheupe