Klabu ya Yanga imemtangaza bw. Sead Ramovic Kuwa kocha mkuu wa timu hiyo akichukua nafasi ya Miguel Gamondi aliyetimuliwa hii leo. Kocha Sead haendani na hadhi ya Yanga kuanzia uzoefu wake wa miaka mitatu katika soka mpaka ujengaji wa timu. Kocha huyu amefanya vibaya mno msimu wa 2024/25 baada ya kushinda mechi 1 kati ya 9 alizoiongoza TS Galaxy na hata ukimlinganisha na kocha Gamondi aliyeiongoza Yanga katika michezo 10 ya ligi akishinda michezo 8 na kupoteza miwili pekee.
Pili Kocha Sead Ramovic amekuja kwa mashinikizo ya nani? Ukiutizama msimamo wa ligi ya Afrika Kusini TS Galaxy iko nafasi ya 16 ikishikilia mkia , ligi ya Afrika kusini ni ya 4 kwa ubora Afrika ikipishana kwa nafasi mbili tu na Tanzania inayoshika nafasi ya 6 je kipi kiliwapeleka viongozi wa Yanga kumchukua kocha huyo?
Wengi wanataka kumfahamu kocha huyu mpya ni Nani na anahistoria katika soka?
Sead Ramovic ni nani?
Sead Ramović (aliyezaliwa 14 Machi 2001) ni meneja wa soka wa Ujerumani na mchezaji wa zamani ambaye alicheza kama kipa. Hivi majuzi alikuwa meneja wa timu ya Ligi Kuu ya Soka ya TS Galaxy.
Mzaliwa wa Stuttgart, Ujerumani Magharibi, Ramović alianza uchezaji wake na FC Feuerbach. Tangu wakati huo, amechezea SpVgg Feuerbach, Stuttgarter Kickers, VfL Wolfsburg, Borussia Mönchengladbach, na Kickers Offenbach, ambazo zote ni vilabu vya Ujerumani. Mnamo Julai 2006, alisaini na klabu ya Tippeligaen Tromsø IL. Mnamo 2010, alisaini Sivasspor. Mnamo 2011, alihamia FK Novi Pazar na kucheza katika Superliga ya Serbia. Mnamo tarehe 17 Novemba 2011, ilitangazwa kuwa atajiunga na Lillestrøm SK kwa msimu wa 2012. [5]
Kufuatia matumizi machache na Vendsyssel katika msimu wa 2013, Ramović alijiunga na Strømsgodset kabla ya msimu wa 2014, lakini alistaafu kutoka kwa timu mapema katika msimu, tarehe 21 Mei. [4]
Kuitwa timu ya Taifa kama mchezaji
Ramović alipokea mwito wake wa kwanza kujiunga na timu ya taifa ya kandanda ya Bosnia na Herzegovina mwaka wa 2004. [6] Ingawa alijumuishwa kwenye kikosi mara kadhaa, hakuwahi kupata mechi.
Taaluma na uzoefu wake wa Ukocha
Sead Ramovic anamiliki leseni ya UEFA pro Licence na hutumia mfumo wa 4-2-3-1 kama Miguel Gamondi.Kocha huyu anamiaka 3 tu tangu awe Kocha rasmi akiitumikia klabu ya TS Galaxy ya nchini nchini Afrika kusini timu inayocheza ligi daraja kuu. Kocha huyo ameiongoza TS Galaxy katika michezo 76 akishinda 27 sare 22 na vipigo 27 akifunga mabao 82 na kufungwa 68 akiwa na Clean sheet 31.
Matokeo mabaya kwa msimu wa 2024/25
Kocha Sead Ramovic ameiongoza TS Galaxy katika michezo 9 ya mashindano mbalimbali akishinda mchezo mmoja pekee. Michuano aliyoshiriki msimu huu ni Betway Premiership mechi 6 akipoteza mechi 4 na sare 2. Michuano ya Carling Knockout mechi 2 akishinda 1 kupoteza 1 na MTN8 mechi 1 na akapoteza mechi hiyo.