Utoaji wa msaada wa kifedha kwa ajili ya kusaidia walioathirika baada ya kuporomoka kwa Jengo la Ghorofa lililopo Kariakoo Jijini Dar es Salaam, utaelekezwa kwenye akaunti maalum ya maafa namba 9921159801 ambayo ipo BoT na inashughulikiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Kauli hiyo, imetolewa hii leo Novemba 18, 2024 Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. Jim Yonazi wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu hali inayoendelea katika zoezi la uokoaji.
Amesema, “Akaunti hiyo ni pekee nchini ambayo inakusanya misaada ya kifedha kwaajhili ya maafa. Kuna watu wana nia njema kabisa kwaajili ya kuwasaidia Watanzania, lakini naomba tujizuie kabisa kukusanya michango ya kifedha kutoka kwa mtu yeyote bila kupitia akaunti hii.”
Dkt. Yonazi ameongeza kuwa akaunti hiyo ni maalumu imethibitishwa na serikali, ili kuweza kuhakikisha misaada inawafikia walengwa na inatimiza malengo ya kutoa misaada hiyo na kwamba kwasasa operesheni inaendelea mpaka pale watakapokamilisha zoezi la kuwaokoa watu ambao bado hawajatoka kwenye jengo hilo.

Polisi: Mnaolala Nyumba za Wageni andikeni taarifa sahihi
Acheter du Viagra en toute sécurité : Guide pratique et conseils