Katika kuhakikisha hali ya usalama inaendelea kuimarika katika maeneo mbalimbali ya Kata ya Mahenje, Elimu ya ushirikishwaji wa jamii imeendelea kutolewa na Polisi Kata wa kata hiyo, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Nelson Mwinuka kwa kutembelea Nyumba kulala Wageni zilizopo Kata hiyo ya Wilayani Mbozi Mkoani Songwe.
Akiwa katika maeneo hayo, Mkaguzi Msaidizi Mwinuka alitoa elimu ya ulinzi jirani na ulinzi shirikishi kwa Wahudumu wa Nyumba za kulala Wageni, juu ya umuhimu wa mteja kujaza taarifa sahihi kwenye vitabu vyao, huku akiwasitiza kupata taarifa sahihi za kila mgeni.
Aidha, amesema Wageni hao wahakikishe taarifa wanazotoa zinafanana na vitambulisho vyao, ili kuweza kubaini mgeni ambaye anaweza kuwa ni hatari kwa usalama na kwamba watu wa jinsia moja wasiruhusiwe kulala chumba kimoja na taarifa za unyanyasaji wa kijinsia ni lazima ziripotiwe bila kificho.