Johansen Buberwa – Kagera.

Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo cha Ualimu Katoke kilichopo Wilayani Muleba Mkoani Kagera, wameiomba jamii kuendelea kuenzi mila, tamaduni na desturi za kiafrika zinazotambulisha asili yao, pamoja kuotaka Serikali kuendelea kuunga mkono tamaduni hizo.

Wakizungumza baada ya kumalikiza kwa Bonanza lililofanyika ndani ya chuo hicho, Wanafunzi hao wamesema jamii inatakiwa kuenzi tamaduni walizo asisiwa na wazee wao ikiwemo kutumia vyakula vya asili kama ambavyo Mkoa wa Kagera unavyolipatia thamani na heshima zao la ndizi.

“Baada ya Sayansi na teknolokia kuendelea imeonekana baadhi tamaduni zimesahalika ukiangalia upande wa mabinti na wakina mama baadhi yao hawajihi kumenya ndizi baada ya kuathiliwa na teknoloknolojia iliyopo tungependa kuishauri jamii wazazi waendelee kuenzi tamaduni kwa kuwafundisha watoto wa kike na kiume,” wamesema Wanachuo Katoke Simeo, Velediana na Happiness.

Naye Mkufunzi wa Chuo hicho, Suzan Mwaimu amesema shindano hilo la umenyaji wa ndizi kwa njia ya asili umezingatia vigezo ambavyo wahenga walivifuata kwanza ndizi ambayo ilimenywa kwa kutumia mti aina ya muanzi unachongwa au matete.

Amesema, “mti wowote ambao unaweza kuchongwa kwa ncha kali ili uweze kumenya ndizi pili ndizi inaanza kumenywa maganda ya juu magumu ukifatishwa maganda ya ndani ili ndizi ibaki kuwa safi na tatu ndizi ya kihaya ukisha imenya lazima uikate vipande kadhaa kulingana na urefu wa ndizi.”

Ameongeza kuwa, “kuna ndizi aina ya enjoboo unakata hata vipande hata sita maana ni ndefu sana kana nyingine aina ya nshakara unaweza kukata vipande zaidi ya vitatu na zaid na ndizi aina ya ntobe fupi kuliko zote hiyo lazima utakata vipande viwili vidogo ambapo ndizi ya kihaya iwe na ufupi kiasi gani haurusiwi kupika ikiwa imenyooka nzima nzima.”

Suzan amendelea kusema Bonanza hilo pia lilishindanishwa wanachuo sita na akapatikana mashindi wa kwanza Happiness Willson aliyekidhi vigezo kwa kumaliza kumenya ndizi alizopewa hiyo ikiwa ni njia mojawapo ya kuimarisha mila na desturi zinazoanza sahaulika.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Novemba 19, 2024
Maendeleo yachangia ongezeko mahitaji ya Umeme - Kapinga