Humphrey Edward.

Leo Novemba 19, 2024 Dunia inaadhimisha siku ya Choo inayoenda sambamba na kaulimbiu ya kuongeza kasi ya mabadiliko, huku wavumbuzi wakiwa ni sehemu ya juhudi zinazoendelea za kushughulikia mahitaji ya takriban watu bilioni 3.5 duniani wanaoishi bila vyoo salama.

Siku hii huadhimishwa kama njia mojawapo ya kuhimiza umuhimu wa usafi wa Mazingira na upatikanaji wa Vyoo vya kutosha, kwani Watu wanaokosa huduma za Vyoo Salama wengi wao huathirika Kiafya na kupelekea uwepo wa uchafuzi wa Mazingira.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa – UN, Watoto 1,000 hufariki kila mwaka kutokana na Magonjwa ya Kuhara yanayosababishwa na matumizi ya Maji machafu, licha ya uwepo wa juhudi za Serikali za Mataifa za kufanikisha utoaji elimu na hamasa kwa wananchi kujenga Vyoo bora na salama.

 

Aidha, ripoti ya   ya mwaka 2019 ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto – UNICEF, ilionesha takriban Watu Bilioni 2 Duniani wanatumia vyanzo vya Maji ya kunywa vilivyochafuliwa na Kinyesi, huku nusu ya Shule Duniani zikikosa Maji Salama na Sabuni.

Kwa hapa nchini taarifa zinaonesha kuwa Taifa limepiga hatua kutokana na ongezeko la uwepo wa Vyoo bora, huku kaya zisizokuwa na huduma hiyo zikipungua kwa kiwango kikubwa.

Hata hivyo, kiuhalisia haya si mafanikio kwani bado wadau wa mazingira na Afya kiujumla wanatamani kutosikia juu ya uwepo wa mtu au jamii iliyoachwa nyuma katika suala zima la matumizi ya Choo bora na salama kwani Choo duni ni hatari na kinaweza kusababisha mlipuko wa magonjwa mbalimbali, ikiwemo kipindupindu.

Ni wazi kuwa,  jamii inabidi iongeza ushirikiano na Watunga sera, Watu wa rasilimali za Maji, Wataalamu wa usafi wa Mazingira na Watendaji, ili suala la umiliki wa choo bora lisionekane kama ni anasa, bali ni hitaji muhimu katika maisha ya Mwanadamu.

Maagizo mapya ya Rais Samia Jengo lililoporomoka Kariakoo
Maisha: Hii hapa mbinu ya kupata Tenda kiurahisi