Johansen Buberwa – Kagera.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi wa Chama cha Mapinduzi – CCM, Taifa na Mjumbe wa Sekretarieti ya Halmashari Kuu, Ally Salum Hapi anatarajia kuzindua kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mkoa wa Kagera Novemba 20, 2024.

Akizungumza na Vyombo vya Habari hii leo Novemba 19, 2024 kwenye ofisi za Chama hicho Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi Mkoa wa Kagera, Hamim Mahmoud amesema Kampeni hizo zinatarajiwa kufunguliwa katika viwanja vya Kashai vilivyopo Manispaa ya Bukoba.

Amesema mbali na uzinduzi, Kiongozi huyo pia atawatambulisha za Wagombea wote wakiwemo Wajumbe wa Viti maalumu, Wajumbe mchanganyiko na Kamati za Mitaa.

Aidha, Mahmoud amesema zoezi hilo litaendeshwa kwa kushirikiana na Viongozi wa CCM Mkoa na Wilaya, huku akiwataka Wananchi na WanaCCM kujitokeza kwa wingi kushuhudia uzinduzi huo wa Kampeni.

Таза тұқымды иттердің Entrefile аудиті: RKF-мен онлайн автокөлік қызметі
Mapenzi, Elimu ni vitu viwili tofauti - Koplo Machuma