Afarah Suleiman, Simanjiro – Manyara.

Mkoa wa Manyara umezindua Kliniki Maalum ya kwanza ya Madaktari bingwa kwa kutumia Madaktari bingwa wa ndani, ili kutoa huduma bobezi za kitabibu za Magonjwa mbalimbali, yakiwemo ya Wanawake na Watoto, Kisubiri, Saratani na Shinikizo la juu la Damu.

Akizindua rasmi Kliniki hiyo ya kwanza kwa ngazi ya Mkoa ya Madaktari Bingwa na bobezi kufanyika kwa ngazi za Mikoa katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Cuthbert Sendiga amesema Kliniki hiyo itadumu kwa siku tano kuanzia November 19 – 22, 2024.

Amesema, Kliniki hiyo itasaidia kupunguza gharama za matibabu kwa Wananchi kusafiri kwenda mbali kuwafuata Madaktari Bingwa na bobezi, kwani gharama zake ni zilezile zinazotolewa kwenye Hospitali za Wilaya na hakuna nyongeza yoyote.

Baadhi ya Wananchi waliojitokezea katika uzinduzi huo wameushukuru uongozi wa Mkoa kwa ubunifu huo na kushauri kuwa iwe ni endelevu na ifike katika halmashauri zote.

Uchaguzi: Viongozi Vyama vya Siasa waaswa kudumisha amani
Hatma ya Guardiola mikononi mwa sheikh Mansoor,Mwenendo mbovu kumponza?