Brentford wanakabiliwa na tishio la kumpoteza Bryan Mbeumo, kocha wa Manchester United Ruben Amorim anataka kuungana na Ousmane Diomande, West Ham huenda wakakatiza uhusiano wao na Guido Rodriguez.
Beki wa Sporting na Ivory Coast Ousmane Diomande, 20, amezungumza na Ruben Amorim wa Manchester United kuhusu kuungana tena na kocha wake wa zamani Old Trafford. (Metro)
Manchester City wapo katika nafasi nzuri ya kumpata kiungo wa Bayer Leverkusen Florian Wirtz, 21, huku Real Madrid na Liverpool zikimkosa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani. (Caught Offside)
Beki wa klabu ya Santos Joao Victor de Souza, 18, ananyatiwa na Chelsea lakini klabu hiyo ya Ligi ya Premia itakabiliwa na ushindani kutoka kwa Barcelona kumnunua Mbrazil huyo. (AS – kwa
Liverpool na Newcastle wanavutiwa na mshambuliaji wa Brentford na Cameroon Bryan Mbeumo, 25. (Sun)
Ajenti Jorge Mendes anajaribu kupata uhamisho wa winga wa Sporting wa chini ya umri wa miaka 21 wa Ureno Geovany Quenda, 17, huku akitarajiwa kutua Manchester United. (Team Talk)
Kiungo wa kati wa Rosenborg na Norway Sverre Nypan, 17, hatajiunga na Manchester United hadi atakapohakikishiwa kuhusu soka la kikosi cha kwanza. (Give Me Sport)
Aliyekuwa mkufunzi wa muda wa Manchester United Ruud van Nistelrooy ana nia ya kusalia kwenye Ligi ya Premia huku kukiwa na nafasi za ukocha katika klabu za Southampton, Wolves na Crystal Palace. (Football Insider)
West Ham wako tayari kumuuza mchezaji aliyesajiliwa katika majira ya kiangazi Guido Rodriguez, 30, mwezi Januari, na kurejea katika klabu ya zamani ya Real Betis kumsaka kiungo huyo wa Argentina. (Estadio Deportivo – kwa Kihispania)
Southampton, Brighton na Ipswich wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Vasco de Gama raia wa Brazil Rayan, 18, mwezi Januari. (Give Me Sport)
Nottingham Forest itahitaji zaidi ya pauni milioni 70 kumnunua beki wa Brazil Murillo, ambaye anawindwa na Liverpool. (Football Insider)
Manchester City wako tayari kumenyana na Paris St-Germain na Juventus kumnunua kiungo wa kati wa Atalanta na Brazil Ederson, 25. (Calciomercato – kwa Kiitaliano)
Besiktas wanatumai kumsajili kiungo wa kati wa Italia Jorginho, 32, bila malipo kandarasi yake na Arsenal itakapokamilika msimu huu. (Sabah – kwa Kituruki)
West Ham, Brighton na Fulham wanamfuatilia kiungo wa kati wa Uingereza Josh Brownhill, 28, ambaye bado hajasaini mkataba mpya na Burnley. (TBR)