Boniface Gideon, Handeni – Tanga.

Chama cha The Nation League For Democracy (NLD), kimezindua rasmi kampeni zake kuelekea Uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024 huku kikiwa na agenda lukuki ambazo zitasaidia kuongeza wigo wa ajira na Maendeleo Nchini,na kulaani vikali Serikali kuwatumikisha kazi ngumu ikiwemo kuchimba mitaro,visima na mabwawa kwa Wanachama wa TASAF.

Katika uzinduzi wa kampeni hizo uliofanyika katika Kijiji cha Kwedikwazu Wilayani Handeni, Katibu Mkuu wa NLD, Doyo Hassan Doyo amesema wamesimamisha wagombea kwenye mitaa na vijiji zaidi ya 700 nchini na wanatarajia kupata ushindi katika maeneo yote yenye Wagombea.

Katibu Mkuu wa Chama cha The Nation League For Democracy (NLD), Doyo Hassan Doyo akizungumza na Wakazi wa Kijiji cha Kwedikwazu Wilayani Handeni Mkoani Tanga wakati wa uzinduzi wa kampeni za Uchaguzi wa Serikali za mitaa, utakaofanyika Novemba 27, 2024.Amesema, “Chama chetu kimesimamisha wagombea kwenye mitaa na vijiji vingi nchini, kwa Kijiji hiki tumesimamisha wagombea kwenye mitaa yote na wajumbe, pia Wilaya yetu tumesimamisha wagombea kwenye mitaa na vijiji karibu maeneo yote, tunatarajia kuchukua ushindi katika maeneo yote kwani tumesimamisha wagombea wanaokubalika.”

Doyo ameongeza kuwa, “Kijiji hiki kina madini lakini kwenye account ya Kijiji hakuna hata mia Mbovu,mana yake uongozi uliokuwepo madarakani umeshindwa kusimamia maslahi ya Wakazi wa Kijiji hiki,sisi NLD tukiingia madarakani tutahakikisha Kijijiji hiki kinapata mapato kutokana na madini ,tutajenga ofisi nzuri ya Kijiji pamoja na Madarasa mazuri yakusomea.”

Wakazi wa Kijiji cha Kwedikwazu wilayani Handeni Mkoani Tanga, wakiwa kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za Uchaguzi wa Serikali za mitaa.

Kuhusu kutumikishwa kazi ngumu kwa wanufaika wa TASAF,Doyo alisema, Serikali imekuwa na tabia yakuwatumikisha Wanachama wa TASAF kufanya kazi ngumu na kuahidi yupo tayari kuwalipia kila Mzee Sh.30,000 kila mwezi bila kufanya kazi ngumu.

“Serikali yetu imekuwa ikiwatumikisha kazi ngumu wazee wanaopata fedha za TASAF, wanachimba mabwawa, kuchimba mitaro, visima nk, lakini pia kwenye Wanachama wa TASAF wamo vijana Wenye umri mdogo kitu ambacho ni kinyume na malengo, lengo la TASAF ni kusaidia Kaya Maskini hususani wazee, lakini wazee hao ndo wanatumikishwa kazi ngumu,” aliongeza Doyo.

Karagwe: DC Laizer aipongeza BUWASA usimamizi Miradi ya Maji