Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia Katibu wa UWT Taifa Suzan Kunambi, amewataka Wananchi wa Kata ya Kilimani Mkoani Dodoma kutopuuzia upigaji kura katika uchaguzi wa Serikali za Mita, ili kuchagua Viongozi bora.

Akizungumza na Wananchi wa Kata hiyo leo Jijini Dododom amesema CCM hakijawai kudharau chaguzi na kila mtu anahaki ya kupiga kura.

Amesema, “sisi Chama cha Mapinduzi hatujawai kudharau kura ya mwananchi, tunaheshimu chaguzi zenu na ndiyo maana hatujawai kushindwa, tuache kufanya mzahaha, sisi chaguzi sio mdhaha, tusifanye mchezo huo, na kata hii ya kilimani ni kata ya heshima, Viongozi karibu wote wa chama wanaishi hapa kwahiyo tunapaswa kushinda ushindi wa heshima.”

Hata hivyo, amempongeza Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu kwa mageuzi makubwa ambayo anaendelea kuyaleta katika ngazi za Kata.

“Tunaendelea kunufaiki na SGR, tunaona mageuzi ya mtu mmoja mmoja, kwenye suala la usafirishaji tumerahisishiwa na hii yote ni kupitia chama hichi,” amesema Kunambi.

Kapinga aendeleza mchakamchaka kuhamasisha ushiriki wa Uchaguzi
Tanzania, Uganda kuendelea kuimarisha ushirikiano