Johansen Buberwa – Kagera.

Wanachi wa Kata Bilele Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera, wamepoke zaidi ya shilingi Bilion 11.8 katika huduma mbalimbali pamoja na miundombinu kutoka Serikalini.

Hayo yamebainishwa na Diwani wa kata ya Bilele, Tawfiq Sharif wakati akiwanadi wagombea 24 wakiwemo Wenyeviti wanne na Wajumbe mchaganyiko wa kwenye kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa.

Amesema, “tumepata maendeleo zikiwemo taa za barabarani, hospital ya Rufaa, Jengo la wangonjwa mahututi kwa Bilioni 770, vitanda vipya vya Wagonjwa kwenye kituo cha Afya Zam Zam kwa milioni 31.8 na hospital ya Mkoa mashine mpya ya Scan pamoja na jengo lake.”

Tawfiq ameongza kuwa, “haya yote ni matoke ya kuchagua viongozi tunao elewana tumekuja hapa ndugu zangu kuwaomba kura mtuchague sisi Viongozi wa CCM.”

Katika hatua nyingine Diwani huyo amesema muda sio mrefu kupitia kwa viongozi wa Mkoa huo akiwemo Mkuu wa Mkoa Hajjat Fatma Mwassa na Mstahik meya manispaa ya Bukoba Godson Gpyson Stendi ya Mabasi itamalizika.

Kwa upande wa wagombea wa Chama hicho wameendelea kuomba ridhaa kwa Wananchi akiwemo Mjumbe wa mkutano kuu CCM taifa Almasud Kalumuna aliyesisitiza Wananchi wawapigie wagombea kwani wamefanya maendeleo mazuri yanayoonekana.

Wafugaji wapewa mbinu kudhibiti UVIDA
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Novemba 26, 2024