Lydia Mollel – Morogoro.
Mkurugenzi Huduma za Mifugo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi amewathimiza Wafugaji wa Mifugo na Ndege wa majumbani kote nchini, kuzingatia kanuni bora za ufugaji, kwa kuepuka matumizi holela ya dawa za mifugo ili kulinda afya za watumiaji wa mazao ya mifugo hiyo ambao wapo hatarini kukabiliwa na Usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya Dawa.
Amesema serikali imefanya jitihada kubwa kutengeneza mazingira mazuri kupitia uwekezaji na kila mmoja kujingizia kipato katik shughuli wanazozifanya, lakini baadhi ya watu hasa wafugaji wa kuku na Nguruwe na mifugo mingine, baadhi yao hawazingatii kanuni za ufugaji, kuku ana siku 4 tu washamjaza dawa, matokeo yake walaji wanapata athari ya Usugu wa Vimelea Vya Magonjwa Dhidi ya Dawa.
“Serikalli itaendelea kuwajengea uwezo wafugaji kujikita katika ufugaji pasipo kutumia dawa na tija ikapatikana katika shughuli wanazofanya, akihimiza wafugaji kote nchini kuwa sehemu ya kamoeni hii ili kulinda afya za walaji wa mazao ya mifugo,” amesema.
Katika Wiki la Maadhimisho ya Usugu wa Vimelea vya Magonjwa dhidi ya Dawa huko mkoani Morogoro, Mratibu Mradi wa UVIDA hapa nchini kutoka Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO) Dkt. Elibariki Mwakapeje, anasema asilimia 80 ya dawa zinazotumika kwa mifugo hutumika pia kwa binadamu, kutozangatiwa kwa matumizi hupelekea UVIDA kwa walaji, na sasa wana mashirikiano na Taasisi mbalimbali ikiwemo Chuo cha Afya cha Hermags kuendelea kutoa elimu kwa jamii.
Usugu wa Vimelea vya Magonjwa dhidi ya Dawa ni moja ya changamoto inayoendelea kukua kwa kasi Tanzania na Duniani kwa ujumla, ambapo kwa mwaka zaidi ya vifo vya watu 2,500,000 kote duniani hutokea kwasababu ya changamoto hiyo hali ambayo inaifanya Tanzania kuungana na Mataifa mengine kudhibiti UVIDA