Afarah suleiman – Simanjiro Manyara.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Cuthbert Sendiga, amezindua huduma za awali za jengo la mama na mtoto katika zahanati ya Oltotoi kata ya Loiborsiret Wilayani Simanjiro mkoani humo
Sendiga amesema Zahanati hiyo inayojengwa kwa gharama ya Tshs 153,029,820/= ikiwa ni sehemu ya fedha shilingi milioni 300 zilizotolewa ili kuboresha hali ya upatikanaji huduma Afya kwenye eneo hilo la jamii ya wafugaji.
Akizindua huduma hizo za awali za jengo la mama na mtoto, Sendiga ameelekeza Halmashauri ya Simanjiro kukamilisha Zahanati hiyo Desemba 2024 na huduma zote muhimu zianze kutolewa ukiacha huduma za Mama na mtoto ambazo ambazo tayari zimeanza kutolewa baada ya uzinduzi.
Aidha, Sendiga ameeleza mpango wa Serikali katika kuendelea kuboresha na kufikisha huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo Afya, maji, umeme, barabara na mawasiliano katika Kijiji hicho.
Nao baadhi ya Wananchi wa kijiji cha kimatoro wilayani simanjiro mkoani manyara wameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wake dkt.samia suluhu hassan kwa kuwajengea zahanati katika kijiji hicho,ambayo itasaidi kuokoa maisha ya watu kwa kuepusha kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya.