Johansen Buberwa – Kagera.
Ikiwa ni siku ya kufunga kampeni za uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024 Meya wa Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera, Gpyson Godson aishukuru Serikali kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye kata Nshambya.
Akizungumza wakati akiwanadi wagombea wa Chama cha mapinduzi – CCM, Godson amesema kwenye kata hiyo wamepokea zaidi ya shilingi bilion 8 kwa utekelezaji miradi ya mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Afya,Elimu na Barabara.
Ameswma, “Hospital ya wilaya,Omani sekondari mabweni manne yamejengwa shule ya Sekondari Nshambya madarasa 13 yamejengwa barabara hayo yote yametekelezwa na viongozi wetu hawa wanaogombea naomba wananchi viongozi hawa muwapatie kura za ndio ili tuendelee kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi.”
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini, Wakili Stephano Byabato ameawasa Wananchi wa kata hiyo wajitokeze kwa wingi na kuchagua viongozi wa CCM, ili waendelee kupata maendeleo.