Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mwalimu Fakii Lulandala ameipongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wake Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za miradi ya maendeleo ikiwepo miradi ya Afya, Maji, pamoja na Barabara katika Wilaya hiyo.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa huduma za awali za jengo la mama na mtoto katika zahanati ya Oltotoi kata ya Loiborsiret Wilayani humo Lulanda amesema alitoa maelekezo Novemba 12, 2024 juu utekeleza wa jengo hilo kukamilika kabla ya Desemba 1, 2024.

Zahanati hiyo inayojengwa kwa gharama ya Tshs 153,029,820/= ikiwa ni sehemu ya fedha shilingi milioni 300 zilizotolewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha hali ya upatikanaji huduma Afya kwenye eneo hilo la jamii ya wafugaji.

Nao Wananchi wa kijiji cha kimatoro wilayani simanjiro mkoani manyara wameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wake dkt.samia suluhu hassan kwa kuwajengea zahanati katika kijiji hicho,ambayo itasaidi kuokoa maisha ya watu kwa kuepusha kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya.

Kapinga: Tujitokeze kwa wingi kupiga kura Novemba 27, 2024
Byabato, Godson wauwasha moto hitimisho la Kampeni Kagera