Mkurugenzi Mteule wa Shirikika la Afya Duniani Kanda ya Afrika – WHO, na Mbunge wa jimbo la Kigamboni, Dkt. Faustine Ndugulile amefariki.

Dkt. Ndugulile amefariki usiku wa kuamkia leo Novemba 27, 2024 Nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu na taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Spika wa Bunge, Dkt  Tulia Ackson.

Amesema, “nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile.”

Spika Tulia ameongeza kuwa “Kwa niaba ya Wabunge natoa pole kwa familia, wakazi wa Kigamboni na Watanzania wote. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.”

Uchaguzi: Kailima apiga kura, awapa ujumbe Watanzania
Kero ya Maji Handeni yaichefua NLD, yaahidi kuitatua