Chama cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA, Jimbo la Babati Mjini Mkoani Manyara kimelalamikia kuenguliwa na kuondolewa kwa mawakala 63 katika vituo vya kupiga kura kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa kwa madai ya mawakala hao kutokua na sifa.
Malalamiko hayo, yametolewa na Mwanasheria wa CHADEMA jimbo la Babati Mjini na Kanda ya Kaskazini, Thadey Lister na Mawakala wa Chama hicho.
Hata hivyo, Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Babati mjini ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati Shaaban Mpendu amekanusha madai hayo na kusema Mawakala walioenguliwa ni wale ambao ni wagombea Uenyekiti.