Mkuu wa Wilaya ya Kibiti, Kanal Joseph Kolombo amekabidhi kwa wananchi visima vinne vyenye thamani ya zaidi ya bilioni moja baada ya kukamilika na kuanza kuhudumia wananchi wilayani humo kati ya visima 900 vya mradi was maji wa Mama (Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan) alivyotoa nchi nzima.
Kanal Korombo amekabidhi visima hivyo wakati akiwa katika ziara yake ya siku moja ya uzinduzi na kukabidhi miradi hiyo kwa wananchi katika vijiji na Kata za wilaya hiyo kwa ushirikiano wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini RUWASA wilaya ya Kibiti.
Amesema Dkt. Samia ametoa visima 900 kwaajili ya kumaliza kero ya maji vijijini nchi nzima ambapo kwa wilaya ya Kibiti imepata mgao wa visima hivyo vitano kwa lengo la kumtua mama ndoo kichwani.
Kanal Korombo amevitaja vijiji vilivyonufaika na mradi huo wa visimavya mama ni pamoja na kijiji cha Mangwi, Nyamatanga, Rungungu, Nyakaumbanga, Pagae na kuwataa wananchi hao kuvitunza visima hivo ili kuweza kuwanufaisha zaidi kwa muda mrefu, hata kufikia makadirio ya miaka kudumu kwa visima hivo ni miaka 50.
Aidha DC kanal Korombo amesema visima hivyo vitano ni miradi mikubwa ambayo itanufaisha idadi kubwa ya wananchi wilayani humo kwani visima vikubwa na vyote vinatoa maji vizuri.
”Tunashukuru sana kwa miradi kama hii mikubwa niwasihi wananchi wa wilaya ya Kibiti tuliopewa miradi hii tuendelee kuilinda, maji haya tuyatumie hata miaka 50 mbele maana yake watoto wetu wayakute maji haya sio tuyatumie tu sisi watu wazima”
”Watoto wetu wayakute maji haya watakapouliza waambiwe maji haya yalichimbwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan watakapokuwa watu wazima,”
”Niwaombe watu wa Kibiti tuvilinde visima hivi vitumike muda mrefu watoto wetu waendelee kutumia maji haya,” alisema Kanal Korombo.
Aidha aliishukuru serikali kwa kuwajali wananchi wa Wilaya ya Kibiti kwa kuwaletea miradi mingi ambapo katika sekta tu ya maji kuna miradi mingi ya mai sio tu visima hivyo vitano vya mama”
‘Miradi yote inatoa maji, ukienda sekta ya elimu, afya note kuna miradi inaendelea hivyo tuna vitu vingi vya kuishukuru serikali ya Mheshimiwa Dkt. Samia” alisema Kanal Korombo.
Kwa upande wake Meneja wa RUWASA Kibiti Ramadhani Mabula katika taarifa ya mirai hiyo amesema kuwa miradi hiyo ilianza kutekelezwa rasmi tarehe 02 October 2024 na ilitarajiwa kukamilika Disemba 30 mwaka huu lakini imekwishakamilika na kukabidhiwa kwa wananchi.
Alisema kukamilika kwa miradi hiyo kutasaidia kuchochea maendeleo kwa wananchi ikiwa ni pamoja na wananchi zaidi ya.13000 wanatarajia kuhudumiwa na miradi hiyo ya maji wilayani Kibiti mkoani Pwani.
Eng. Mabula alisema faida nyingine ya kukamilika kwa miradi ya visima hivyo kuwa ni pamoja na kupunguza magonjwa yanayotokana na uhaba wa majina kuwapa wananchi wepesi wa maisha kwa kuongeza kipato kwa wananchi wa vijiji ambavyo miradi hiyo imepita, wananchi pia walipata ajira kama saidia fundi na vibarua, mama lishe.
Wananchi wametoa shukurani zao za dhati kwa kukamilika kwa miradi hiyo kwani wengi wao walikuwa wakitumia muda wa hata zaidi ya nusu saa hadi Lisa kufata maji visimani lakini sasa huduma hiyo ipo nyumbani kwao.