Johansen Buberwa – Kagera.
Kiwango maambukizi ya virusi vya ukimwi ndani ya manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera kimeendelea kupungu kutoka asilimia 2.2 mwaka 2023 mpaka kufikia asilimia 0.9 kwa kipindi cha januari hadi Octoba mwaka 2024.
Akizungumza katika siku ya Ukimwi duniani iliyoadhimishwa hii leo Desemba 1, 2024 Kashai sokoni Mratibu wa Ukimwi wa Manispaa hiyo, Faraja Chaula amesema pia huduma nyingine inayoendelea kutolewa kwenye jamii ni kupatiwa dawa za kufubaza makali ya virusi hivyo.
Amesema, “idadi ya wangonjwa waliogundulika kuwa na virusi vya ukimwi 497 januari hadi Octoba 2024 na jumla ya wateja wapya waliosajiliwa katika huduma (CDC ) na kuanzishiwa huduma ya dawa ya kupunguza makali ya virusi vya ukimwi walikuwa 413 sawa na asilimia 88.4 ya watu walipatikana na virusi vya UKIMWI.”
Kwa upande wake katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Wilaya Bukoba, Hadija Mkelenga ameiasa jamii kuacha ulevi na kuwa mwenza mmoja na kuacha tabia ya kuchepuka, ili kupunguza au kumaliza.
Naye Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo Naibu Meya Manispaa ya Bukoba, Mwajabu Galiatano amesema jamii kwa sasa ishikamane kuwa mstari wa mbele wa mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi.
Aidha, amewasihi Wananchi kuacha tabia za kushiriki mila na desturi potofu za kurithi wajane, kuacha ngono zembe, uzinzi, madawa ya kulevya pamoja na makundi ikiwemo vishawishi.
Katika maadhimisho hayo, Maafisa wa Tasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa- TAKUKURU Mkoa wa Kagera, Manyama Venace na Elizabeth Lisawa wametoa elimu kwa jamii hiyo juu ya sheria ya rushwa namba 11 ya mwaka 2007 iliyofanyiwa marekebisho 2022 ya rushwa ya ngono.
Wamesema sheria hiyo ni kinyume na kifungu cha 25 maana kosa hilo ni la jinai inajumuisha katika makosa ya uhujumu uchumi ikithibitika mahakamani anaweza kufungwa miaka 20 na kuiasa jamii namna ya kuepuka rushwa ya ngono amabayo upelekea baadhi ya wananchi kupata maabukizi mapya ya virusi vya ukimwi.