Paris St-Germain wako kwenye mazungumzo na Mohamed Salah wa Liverpool, timu nne za Ligi ya Premia zinamfuatilia mashambuliaji wa Borussia Dortmund Jamie Gittens, Manchester United na Spurs wanamtaka kiungo wa Eintracht Frankfurt Omar Marmoush.
Paris St-Germain wanajadiliana na mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah kuhusu uhamisho wa bila malipo wakati mkataba wa mchezaji huyo wa Liverpool mwenye umri wa miaka 32 utakapokamilika mwishoni mwa msimu huu. (L’Equipe – kwa Kifaransa)
Arsenal, Liverpool, Chelsea, na Tottenham wanamfuatilia mshambuliaji wa Borussia Dortmund wa timu ya taifa ya Uingereza ya chini ya miaka 21 Jamie Gittens. (Florian Plettenberg)
Manchester United, Tottenham, Barcelona na Paris St-Germain ziliwatuma wasaka vipaji wao kumfuatilia mshambuliaji wa Misri Omar Marmoush mwenye umri wa miaka 25 akiichezea Eintracht Frankfurt katika Ligi ya Europa siku ya Alhamisi. (Mirror)
Bournemouth wako tayari kupokea ofa ya Antoine Semenyo msimu huu, huku Liverpool wakiwa miongoni mwa vilabu vinavyomhitaji mshambuliaji huyo wa Ghana, 24. (Football Insider)
Arsenal wamepiga hatua katika mazungumzo yao na Roberto Olabe wa Real Sociedad ili kumrithi Edu kama mkurugenzi wa michezo wa Gunners. (Footmercato – kwa Kifaransa)
Bournemouth, Brentford na Southampton wanamtafuta mshambuliaji wa Ureno na klabu ya Wolves Fabio Silva, 22, ambaye yuko Las Palmas kwa mkopo. (Fichajes – kwa Kihispania)
Liverpool wanatumai kuwashinda Manchester United katika usajili wa Januari wa beki wa Hungary Milos Kerkez, 21, ambaye Bournemouth ina thamani ya £40m. (CaughtOffside)
Newcastle wako tayari kumuuza beki wa zamani wa Uingereza Kieran Trippier mwenye umri wa miaka 34 mwezi Januari. (Football Insider)
Al-Hilal wako tayari kuchuana na Arsenal kwa ajili ya kumsajili winga wa Las Palmas mwenye umri wa miaka 21 wa Uhispania Alberto Moleiro. (Team Talk)
Luton ilazimika kulipa £1.5m kumfuta kazi kocha Rob Edwards kwa sababu ya mkataba wa miaka minne aliosaini msimu wa joto. (Sun)