PICHA: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameungana na Familia, Viongozi na Waombolezaji katika Ibada ya kuaga mwili wa aliyekuwa mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani -WHO, Kanda ya Afrika, Marehemu Dkt. Faustine Ndugulile katika Viwanja vya Karimjee, vilivyopo jijini Dar es Salaam hii leo Desemba 2, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan alipowasili Viwanja vya Karimjee Dar es salaam Kuongoza Waombolezaji kuaga mwili wa aliekuwa Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Wa Shirika la Afya Duniani Kanda ya Afrika Dkt. Faustine Ndungulile leo Desemba 2, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu Cha Maombolezo wakati wa Misa ya kuaga mwili wa aliekuwa Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Wa Shirika la Afya Duniani Kanda ya Afrika Marehemu Dkt.Faustine Ndungulile Viwanja vya Karimjee Dar es salaam leo Desemba 2, 2024.
Mwili wa aliekuwa Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Wa Shirika la Afya Duniani Kanda ya Afrika, Marehemu Dkt. Faustine Ndungulile ulipowasili Viwanja Karimjee leo Desemba 2, 2024.