Rais wa Marekani, Joe Biden ametangaza kumsamehe mtoto wake Hunter Biden, ambaye alikuwa akisubiri kuhukumiwa katika kesi za kumiliki silaha kinyume cha sheria na kukwepa kulipa kodi.

Hatua ya Biden inakuja kufuatia Hunter (54), alikiri makosa yake yanayomkabili mapema Septemba 2024 kwa kukwepa kulipa kodi katika Mahakama ya Los Angeles, California na hivyo kuepuka kesi ambapo alikuwa akisubiri hukumu yake.

“Hakuna mtu mwenye busara anayeangalia ukweli katika kesi za Hunter anayeweza kufikia hitimisho lolote isipokuwa hili: Hunter alitengwa kwa sababu tu ni mtoto wangu – na hiyo sio sawa,” alisema Rais Biden.

Chelsea na Liverpool zafanya kweli EPL
Madrid yazidi kupaa kileleni Barcelona wakidorola