Barcelona wamerejea kwa kishindo La Liga baada ya ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Mallorca. Ushindi huo mnene unaifanya Barcelona kusalia kileleni kwa alama 37 katika michezo 16 waliyocheza mpaka sasa.

Tathmini ya Mchezo 

Barcelona walianza na Inaki Pena ,Jules Kounde,Pau Cubaris, Martinez na Balde kwenye safu ya ulinzi. Eneo la kiungo liliundwa na Pedri ,Casano ,Raphinha,Dani Olmo na Lamine Yamal .Ferran Torres ndiye aliyesimama kama mshambuliaji wa mwisho katika mfumo wa 4-2-3-1 unaotumiwa na Hans Flick.

Barcelona walipata bao la uongozi dakia ya 12 kupitia kwa Ferran Torres lakini bao hilo lilisawazishwa na Mshambuliaji wa Mallorca Vedat Muriqi dakika ya 43 na kuufanya mchezo huo kwenda mapumziko kwa sare ya 1-1.

Barcelona walirejea kwa kishindo na kupata penati iliyofungwa na Rafinha dakika ya 56 ambaye alirejea tena langoni kwa Mallorca na kuandika bao la tatu dakika ya 74 akimalizia pasi ya Lamine Yamal.

Barcelona walipata bao la nne kupitia wa super sub Frank De Jong dakika ya 79 na bao la tano lilifungwa na Pau Victor akimalizia pasi kutoka kwa Frank De Jong .

Ushindi huu unawarudisha morali kwa wachezaji wa Barcelona baada ya kupoteza michezo miwili na sare moja dhidi ya Las Palmas ,Real Sociedad na Celtavigo.

Namibia yapata Rais wa kwanza Mwanamke
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Desemba 4, 2024