Ruud Van Nistelrooy ameanza vyema kibarua chake cha kuinoa Leicester City kwa ushindi wa maba0 3-1 dhidi ya Westham. Hii ilikuwa ni mechi ya kwanza kwa kocha huyo siku chache baada ya kuachana na Manchester United . Ikumbukwe Van Nistelrooy aliichukua nafasi ya mpito baada ya Manchester United kuvunja mkataba na Erik Ten Hag.

Katika mchezo huo dhidi ya Westham Van Nistelrooy alipata bao la uongozi kupitia kwa Jamie Vardy dakika ya pili ya mchezo na walikwenda mapumziko wakiwa na uongozi wa bao hilo. Kipindi cha pili El Khannous aliweka kimiani bao la pili dakika ya 61 na bao la tatu dakika ya 90 kupitia kwa Daka.Ushindi huo unawafanya Leicester kufikisha alama 13 wakisalia nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi

Kocha huyo aliiongoza United katika michezo 4 ikiwemo kombe la ligi,Uefa Europa League na mechi mbili za EPL kama kocha wa mpito. Katika michezo hiyo alishinda michezo mitatu na sare moja. Leicester walivutiwa na kocha huyo baada ya kuwaondoa kombe la ligi na kuwafunga mchezo wa ligi kuu.

 

Umeme ni Ajenda ya Serikali, tutaufikisha maeneo yote - Kapinga
Namibia yapata Rais wa kwanza Mwanamke