Nottingham Forest inajiandaa kumnunua Evan Ferguson Januari, Real Madrid itasubiri kumsajili Trent Alexander-Arnold kwa uhamisho wa bure, huku klabu kadhaa za Ligi ya Premia zikimuwania Nico Williams.
Nottingham Forest inajiandaa kuwasilisha dau la kumnunua mshambuliaji wa Brighton na Jamhuri ya Ireland Evan Ferguson, 20, mwezi Januari . (Football Insider)
Real Madrid wanataka kumsajili beki wa Liverpool kutoka Uingereza Trent Alexander-Arnold, 26, kwa uhamisho wa bure. (Telegraph – usajili unahitajika)
Liverpool wanapanga kufanya uhamisho wa pauni milioni 91 Januari kwa beki wa Bournemouth mwenye umri wa miaka 21 na Hungary Milos Kerkez na kiungo wa Real Sociedad na Uhispania Martin Zubimendi, 25. (Teamtalk).
Arsenal, Chelsea, Liverpool na Tottenham ni miongoni mwa vilabu vinavyomuwania winga wa Athletic Bilbao mwenye umri wa miaka 22 Nico Williams. (Athletic -Usajili unahitajika)
Barcelona wanamfuatilia mshambuliaji wa Newcastle United na Uswidi Alexander Isak, 25. (Caught Offside)
Manchester United wana nia ya kumsajili beki wa RB Leipzig wa Ujerumani David Raum, 26, na mshambuliaji wa Juventus na Uturuki Kenan Yildiz, 19. (Sky Germany – kwa Kijerumani)
Manchester United wamewasiliana na beki wa Canada Alphonso Davies, 24, ili kutathini nia yake ya kujiunga na klabu hiyo mkataba wake wa Bayern Munich utakapokamilika msimu ujao. (Team Talk)
Leicester City wana nia ya kuimarisha safu yao ya mashambulizi na wana mpango wa kumsajili mshambuliaji mpya dirisha la uhamisho wa wachezaji litakapofunguliwa Januari. (Football Insider)
Barcelona watamenyana na Real Madrid kumnunua beki wa Manchester United na Ureno Diogo Dalot, iwapo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ataonyesha nia ya kuondoka Old Trafford. (Caught Offside)
Kocha wa zamani wa Manchester United Erik ten Hag ananyatiwa na RB Leipzig. (Sun, via Sky Germany)
Winga wa Ivory Coast Amad Diallo, 22, ahuenda akaondoka Manchester United mwezi Januari bila makubaliano mapya na klabu hiyo. (Express)
Manchester United pia inatathmini chaguo lao la kipa iwapo mchezaji wa Kituruki Altay Bayindir mwenye umri wa miaka 26 ataondoka Januari. (Mail – usajili unahitajika)
Tottenham, Manchester City na Chelsea wanavutiwa na kiungo wa AC Milan na Uholanzi Tijjani Reijnders, 26. (Calciomercato – kwa Kiitaliano)
Kocha wa zamani wa Juventus na AC Milan Massimiliano Allegri ni miongoni mwa wakufunzi wanaowania nafasi ya kuinoa West Ham iwapo The Hammers watamtimua Julen Lopetegui. (Calciomercato – kwa Kiitaliano)