Mgombea Urais wa chama tawala cha South West Africa People’s Organisation – SWAPO, Netumbo Nandi-Ndaitwah (72), ameshinda kiti cha Urais nchini Namibia, kwa kupata asilimia 57.31 za kura, na kuwa Rais wa kwanza Mwanamke nchini humo tangu uhuru wa Taifa hilo wa mwaka 1990.

Tume ya Uchaguzi ya Namibia ECN, imesema Netumbo Nandi-Ndaitwah, anafuatiwa katika nafasi ya pili na mgombea wa chama kikuu cha upinzani cha Patriots for Change – IPC, Panduleni Itula aliyepata asilimia 25.5 ya kura zote.

Nandi-Ndaitwah alihudumu kama Makamu wa Rais wa Namibia, cheo alichopata tangu mwaka 2022 lakini kabla ya hapo, alikuwaa kishikilia nyadhifa mbalimbali za uongozi, ikiwa ni pamoja na kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa tangu 2012.

Namibia ina utajiri mkubwa wa Madini ya Urani na Almasi ila wachambuzi wanasema ni watu wachache katika idadi ya watu milioni tatu raia wa nchi hiyo, walionufaika na utajiri huo, katika masuala ya kimiundo mbinu na fursa za ajira.

Van Nistelrooy ameanza kwa kishindo Leicester City
Lamine Yamal arejea na balaa Barcelona ikiisambaratisha Mallorca