Kikosi cha Yanga kimewasili salama nchini Algeria kuwakabili MC Alger kwenye mchezo wa pili wa ligi ya mabingwa Afrika hatua ya makundi raundi ya pili. Yanga walipoteza mchezo wake wa kwanza wa kundi A kwa mabao 2-0 dhidi ya Al Hilal.Yanga wanapaswa kushinda mchezo huo mgumu wa ugenini ili kujiwekea nafasi ya kufuzu robo fainali ya michuano hiyo. Kikosi hicho kinachonolewa na Mjerumani Ramovich kilianza kurejesha makali yake wikiendi iliyopita kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Namungo mchezo wa ligi kuu ya NBC na hiyo ni ishara ya kurudisha morali kwa wachezaji iliyopotea baada ya kufungwa mechi tatu za awali dhidi ya Tabora United 3-1 ,Azam FC 1-0 na Al Hilal 2-0.
Kikosi chawasili Algeria
Kikosi cha wachezaji 26 kikiongozwa na Diarra,Khomeiny ,Mshery ,Mwamnyeto,Job,Bacca,Yao,Kibabage,Kibwana,Boka, Aucho,Mudathir,Mkude,Abuya,Maxi,Nkane,Farid ,Sheikhan,Pacom,Chama,Aziz Ki ,Baleke,Musonda,Mzize na Prince Dube kimewasili Algeria kwa mchezo utakaopigwa tarehe 7 majira ya saa 10:00 usiku.