Klabu ya Simba imeanza safari kuelekea Algeria kwa mchezo wa kombe la shirikisho dhidi ya Cs Constantine mchezo utakaopigwa tarehe 8 Disemba. Simba iliwasili uwanja wa ndege Julius Nyerere na katika hali isiyotarajiwa mchezaji wake Aishi Manula alishindwa kuendelea na safari hiyo kutokana na changamoto za kiafya.
Kupitia kurasa rasmi za Simba waliiandika taarifa hiyo .
NUKUU;
Mlinda mlango Aishi Manula ameshindwa kuendelea na safari baada ya kupata hitilafu ya kiafya dakika chache kabla ya kuanza safari ya kuelekea nchini Algeria tukiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.
Yusuf Kagoma aibua maswali kwa mashabiki wa Simba.
Katika hali ya kushangaza kiungo wa klabu ya Simba SC Yusuph Kagoma amefuta picha zake zote akiwa na klabu yake,pamoja na utambulisho wake Kama mchezaji wa Simba SC katika Mtandao wa Instagram (BIO ).
Ikumbukwe Yusuf kagoma alikuwa akiuguza majeraha ambayo yalimuweka nje ya uwanja katika michezo kadhaa ambayo klabu ya Simba wamecheza.
Pia kiungo huyo hajasafiri na timu ya Simba siku ya Leo kuelekea nchini Algeria kwenye mchezo wa pili wa Simba hatua ya makundi Kombe la Shirikisho dhidi ya CS Constantine.