Johansen Buberwa – Kagera.

Baadhi ya Majeruhi wa ajali ya Magari matatu yaligongana Wilayani Karagwe Mkoani Kagera iliyotokea Desemba 3, 2024 wanaendelea kupata matibaba vizuri katika Hospital ya Rufaa Bukoba, huku afya zao zikiimarika.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Bukoba Dkt. Museleta Nyakiroto ameyabainisha hayo wakati akizungumza na vyombo vya Habari hii leo Desemba 4, 2024 na kusema jana majira ya saa nane hadi tisa wilipokea idadi ya majeruhi wanane kati yao wanne, Wanaume wakiwa wanne na Wanawake watano na kati ya Wanaume hao kuna mtoto wa miaka sita.

Amesema, “kati yao wanne walivunjika mifupa kwenye miguu na mikono na mtoto alipata maumivu ya kichwa na wengine watatu walikuwa na michubuko na maumivu katika sehemu mbalimbali za mwili wote kwa ujumla wanaendelea na Matibabu hali zao zinaedelea vizuri.”

Wakisimulia tukio hilo, baadhi ya majeruhi akiwemo Dereva wa Hiace Edward Benedicto na Jonas Kivuye wamesema kosa lililofanyika nu wahusika kufungua kizuizi kuruhusu Lori kupita eneo ambalo magari ya abilia yalikuwa yamesimama na dereva wa gari kubwa alijaribu kawakwepa lakini haikuwezekana.

“Wale wanaoruhusu belia wangeruhusu kufungua upande wa kulia Lori lingepita sasa walifungua upande wetu wa kushoto na yule Dereva wa gari alijaribu kutukwepa sisi na mimi nikatoa kichwa hivi Hiace yangu iligongwa na tela kwa nyuma,”

“nilishutukia tuko chini nikajaribu kufungua mlango lakini mguu wangu mmoja ulikuwa umebanwa na vyuma mpaka wasamalia wema wakaja maana mguu tuliutoa ukiwa ushakatika,” alisema Benedikto.

Kwa upande wao baadhi ya Viongozi wa Serikali waliofika Hospitali kuwajulia hali majeruhi hao akiwemo Katibu Tawala Wilaya ya Bukoba, Proscovia Mwambi na Kaimu katibu Mkoa Kagera, Bwai Buseko wametoa pole kwa wafiwa na kwa majeruhi.

Dkt. Biteko: Matumizi bora Nishati yawepo kwenye mipango ya Serikali
simba wakumbwa na majanga wakielekea Algeria