Wabunge wanatarajia kuondoka Nchini Desemba 6, 2024 kuelekea Mombasa kwa ajili ya kushiriki mashindano ya 14 ya michezo ya Mabunge yatakayoanza Desemba 7 hadi 17, 2024.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo Desemba 4, 2024 Jijjni Dodoma, Mwenyekiti Wa klabu za michezo Bungenu, Tarimba Abbas amesema tukio hilo litawakutanisha wabunge kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kushiriki michezo mbalimbali, kwa lengo la kujenga ushirikiano, mshikamano na afya kati ya wabunge.
Amesema, “Maandalizi ya mashindano yanaendelea kufanyika jijini Dodoma wanatarajia kuanza safari Ijumaa hii ya tarehe 7 ambapo mazoezi hayo ni sehemu ya juhudi za wabunge kujiweka sawa ili kuhakikisha wanaiwakilisha vyema Nchi katika michezo hiyo.”
“Na michezo hii hufanyika kila mwaka na inajumuisha michezo mbalimbali kama soka, riadha, netiboli, na golf, huku lengo kuu likiwa ni kuimarisha uhusiano wa kikanda kupitia michezo,” amesema Abbas.
Hata hivyo amesema Wabunge wenye ulemavu wanatarajiwa kushiriki mchezo wa vishale au Darts.