Johansen Buberwa – Kagera.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Faris Buruhani amewataka Wanafunzi wa kidato cha nne pindi wanapohitimu masomo yao wajitambue, ili waweze kukabiliana na changamoto za maisha.
Faris ametoa wito huo katika Mahafali ya 14 ya Shule ya Sekondari Katoro Day yenye jumla ya Wanafunzi 134 Wavulana wakiwa ni 72 na Wasichana 62 waliohitimu kidato cha nne.
Amesema, “kuhakikisha mnakabiliana na changamoto na vikwazo vitakavyowakabili mtaani ili kukidhi kiu ya wazazi wenu wanaowategemea kuhakikisha wanasimamia ndoto zako na wala msiogope kujaribu na kujitolea kwa kuwa elimu ya darasani ni msingi wa kuanza safari na kujua kufanikisha lakini safari ya maisha inahitaji kujituma ujasiri na ushirikiano.”
Kwa upande wake Mkuu wa Shule hiyo amesema Shule ya Sekondari Katoro Day ina mpango wa kuendelea kuboresha taaluma shuleni hapo Kwa kuwa ndio lengo kuu la Shule ambayo imefanikiwa kuongeza idadi ya Wanafunzi wanaomaliza na wanaojiunga na kidato cha kwanza.