Boniface Gideon – Tanga. 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo amesema kuwa wanajiosayansi ni nguzo muhimu katika kufanikisha dhana ya Vision 2030: Madini ni Maisha na Utajiri.

Mbibo ameyasema hayo Desemba 4, 2024 Jijini Tanga wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa Wanajiosayansi kwa niaba ya Waziri wa Madini.

Amesema, Wizara ya Madini inatambua nafasi na mchango wa wanajiosayansi katika Vision 2030 hivyo itaendelea kuwatumia kikamilifu ili kuwezesha utekelezaji wa dhana hii.

“Katika kufanikisha Vision 2030, wanajiosayansi wameendelea kutumia utaalamu wao katika kufanya utafiti wa kina wa kijiofizikia kwa kutumia teknolojia za kisasa kwa lengo la kutambua tabia za miamba. Utambuzi huu utawezesha kufanyika kwa tafiti nyingine za jiosayansi zenye kuwezesha kubaini aina mbalimbali za madini yapatikanayo nchini,” alieleza Mbibo.

Mbibo, kwa niaba ya Wizara ya Madini, aliwashukuru wanajiosayansi kwa utayari wao wa kubeba maono ya Vision 2030 na kutoa msaada wa kitaalamu katika kufikia utekelezaji wake.

Kupitia dhana ya Vision 2030, Wizara ya Madini inalenga kufanya tafiti za kina kwa angalau asilimia 50 kufikia asilimia 2030, ukilinganisha na sasa ambako ni asilimia 16 pekee ndiyo imefanyiwa utafiti wa kina kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

Cách bắt đầu sử dụng Internet Sòng bạc địa phương: Sách dành cho doanh nhân từng bước hành động
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Desemba 5, 2024