Boniface Gideon – Tanga.

Shirika la Petroli Nchini (TPDC), limesema linaendelea na Utafiti wa mafuta katika Bonde la Eyasi-Wembere, lililopo katika Bonde la Ufa la Afrika Mashariki, Endapo Utafiti huo utazaa matunda basi unatajwa kuwa utachangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza uchumi wa Taifa kwa kuongeza pato na kupunguza utegemezi wa mafuta kutoka nje ya Nchi.

Meneja wa Mradi wa Utafiti wa Mafuta katika Bonde la Eyasi-Wembere, Sindi Maduhu, aliyasema hayo wakati wa mkutano wa wanajiosayansi kutoka ndani na nje ya nchi, unaofanyika mjini Tanga kwa siku tatu.

Alisisitiza kuwa utafiti huo utakuwa na manufaa makubwa kwa Tanzania na utasaidia kupunguza gharama za kuagiza mafuta kutoka nje ya nchi.

Amesema, “Bonde la Eyasi-Wembere linapita katika mikoa mitano ya Shinyanga, Simiyu, Arusha, Singida, na Tabora, ambapo lina uhusiano wa kipekee na maeneo mengine ya bonde la Ufa kama vile Uganda na Kenya, Nchi hizi tayari zimegundua mafuta.”

Maduhu aliongeza kuwa Tanzania ina matumaini makubwa ya kugundua mafuta kutokana na uhusiano huo na maeneo mengine ya bonde hilo.

“Eneo hili ni muhimu sana kwa Tanzania kutokana na mshikamano wake na maeneo ya Lokicha nchini Kenya, ambapo mafuta yamevunjwa, na Uganda, ambapo wanajenga bomba la mafuta ghafi ili kupeleka mafuta hayo kwenye viwanda vya usafirishaji,” alisema Maduhu.

Kuhusu Maendeleo ya Utafiti wa Mafuta unaoendelea, Maduhu alifafanua kuwa kazi za utafiti zimeendelea kwa hatua nzuri tangu kuanza kwa mradi huu mwaka 2015.

“Hadi sasa,tumefanikiwa kukusanya taarifa muhimu zinazohusiana na uwepo wa mafuta katika eneo hilo, wanatekeleza uchukuaji wa taarifa za mitetemo za mifumo ya 2D ili kubaini maeneo ya kuchimba,” alisema Maduhu

“Baada ya kuchora ramani ya mifumo ya 2D, tutakuwa katika nafasi nzuri ya kujua kama mafuta yapo na kwa kiwango gani hadi sasa, Tanzania haijagundua mafuta,lakini tunatarajia kupata matokeo chanya kutokana na utafiti huu,” alieleza Maduhu

Videojuego Aviator Asia Apuesta dinero real con premios Grand Victory
Finest No-deposit Incentive Codes United states Casinos November 2024