Johansen Buberwa – Kagera.
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Kagera umemkabidhi Nyumba ya vyumba vinne na Cherehani Mama wa Mtoto Asimwe Novath aliyepoteza maisha baada ya kutekwa na kuuwawa kikatili Wilayani Muleba.
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa huo, Faris Buruhani wenyeamemkabidhi Nyumba Judith Richard amesema kwa niaba ya Vijana anakabidhi Nyumba hiyo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 12, zilizochangwa na wadau mbalimbali.
Amesema, “Wadau waliojitokeza kwa kutupatia fedha ili kuwezesha ujenzi na wengine walituwezesha vifaa tulichofinya kwa ujumla wake ilikuwa ni kuinganisha thamani ya vitu vyote kuanzia vifaa pamoja na pesa ilifikia shilingi 12,792,000.”
Naye Mwakilishi wa Chama cha Watu wenye Ulemavu Mkoa Kagera, Frolensi Felician ameipongeza UVCCM kwa kitendo hicho na kuiomba iendelea kuwalinda watu wenye ulemavu hasa walio na ualbino huku akilaani wale wanaowatenda vibaya.
Kwa upande wake Baba mdogo wa Mama Asimwe, Alikadius Stephen amesema jamii ijifunze kutokana na kitendo hicho kwani kitendo cha kumua kikatili Asimwe kimeacha funzo kubwa na majonzi kwa familia.