Rais wa Syria Bashar al-Assad amekimbia nchi hiyo baada ya waasi kuchukua udhibiti wa mji mkuu Damascus.

Waasi hao, wametangaza kuipindua Serikali ya Rais Bashar al-Assad na utawala wa chuma wa kiongozi huyo ambaye amekuwa madarakani kipindi ambacho taifa hilo la Mashariki ya Kati limekuwa likizongwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa zaidi ya miaka 10.

Mapema hii leo Desemba 8, 2024 Kamandi ya jeshi la Syria iliwaarifu maafisa wake kwamba utawala wa Assad umekwisha.

Jeshi hilo pia limesema bado linaendelea na operesheni dhidi ya makundi ya kigaidi katika miji muhimu ya Hama, Homs na Deraa.

Rais Samia ateuwa, afanya mabadiliko ya Viongozi
Kagera: UVCCM wamkabidhi Nyumba Mama Asimwe