Mkoa wa Manyara umeadhimishi siku ya uhuru wa Tanzania bara kwa kupanda miti katika eneo la Hospitali ya Wilaya ya Babati mrara, pamoja na kuwajulia hali Wagonjwa katika Hospitali hiyo.

Akizungumza mara baada ya zoezi la upandaji wa Miti Mkuu wa Wilaya Babati, Emanuela Kaganda amewataka Wanachi kuendela kudumisha uhuru na mshikamano, ili kulinda amani ya nchi yetu.

Amesema, Wananchi wanatakiwa kutumia maadhimisho hayo pia kuwakumbuka mashujaa mbalimbali wa nchi waliopambania uhuru.

Katika hatua nyingine Kaganda ametembelea Wodi za akina mama, Watoto njiti na chumba maalum kilichoboreshwa katika Hospitali ya Mrara huku akijionea maboresho ya miundombinu iliyofanyika.

Shughuli hizo za upandaji wa Miti na Usafi wa Mazingira ni Utekelezaji wa Maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

best name for boy 2856
Upandaji Miti, usafi wa Mazingira kuwa endelevu - DC Lulandala