Mshambulizi wa Uingereza Cole Palmer, 22, anaivutia Real Madrid kwa sababu ya mchezo wake thabiti akiwa Chelsea. (Fichajes – Spanish)
West Ham itaongeza nia ya kutaka kumnunua mshambuliaji wa Brighton na Jamhuri ya Ireland Evan Ferguson, 20, dirisha la uhamisho la Januari litakapofunguliwa. (Football Insider)
Arsenal, Manchester United na Barcelona wako tayari kupigana vikumbo kwa ajili ya kumnasa fowadi wa Lille kutoka Canada Jonathan David, 24, ambaye kandarasi yake inamalizika msimu wa joto. (Mundo Deportivo – Spanish)
Manchester City wako tayari kumuuza mshambuliaji wa Norway Oscar Bobb, 21, au kiungo wa kati wa Uingereza James McAtee, 22, huku wakitafuta kuwashawishi Bayer Leverkusen kuachana na winga wao wa miaka 21 wa Ujerumani Florian Wirtz. (TBR Football)
Meneja wa Manchester United Ruben Amorim anaweza kuwatoa kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen, 32, na winga wa Brazil Antony, 24, ili kuokoa pesa mwezi Januari. (GiveMeSport)
Liverpool wanatumai kuwashinda wapinzani kadhaa wa Uropa kuinasa saini ya beki wa Bologna Mholanzi Sam Beukema, 26. (Teamtalk).
Kiungo wa kati wa Motherwell na Scotland Lennon Miller, 18, pia analengwa na Liverpool na anaweza kupatikana kwa £8m. (Caught Offside)
Beto wa Everton, 26, anaweza kurejea Italia mwezi Januari, huku Torino ikimtaka mshambuliaji huyo wa Guinea-Bissau. (Tuttomercartoweb – In Itali )
Mchezaji wa Atalanta Ademola Lookman, 27, yuko tayari kurejea Uingereza, huku klabu kadhaa za Ligi ya Premia zikimtaka fowadi huyo wa Nigeria. (GiveMeSport), nje
Chelsea itamtuma kiungo wa kati wa Uingereza Omari Kellyman kwa mkopo mwezi Januari ili kumsaidia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 kupata uzoefu wa juu. (Football Insider),
Graham Potter yuko tayari kuchukua kazi ya West Ham mwanzoni hadi mwisho wa msimu, ikiwa watamfuta kazi Julen Lopetegui. (Sportsport)
Tottenham wanatazamiwa kumuunga mkono meneja Ange Postecoglou na kumsaidia raia huyo wa Australia katika dirisha dogo la usajili la Januari, licha ya matokeo mabaya.(Teamtalk),
Manchester United huenda wakapanga vita dhidi ya Arsenal kumnunua Luis Campos, mshauri wa soka wa Paris St-Germain. (ipaper)